Jinsi ya kujikinga na virusi vya Zika

User avatar
Moderator 1
Site Admin
Posts: 13
Joined: Tue Jun 21, 2016 10:45 am
Contact:

Jinsi ya kujikinga na virusi vya Zika

Postby Moderator 1 » Sun Dec 18, 2016 10:39 pm

Kuenea huku kwa kasi kwa virusi vya Zika ndiko kwa karibuni zaidi kati ya magonjwa manne ya virusi yanayoenezwa na mbu mataifa ya Magharibi katika kipindi cha miaka 20, anaandika Dkt Fauci kwenye makala katika jarida la kimatibabu lathe New England Journal of Medicine.

Mlipuko huu unafuata mlipuko wa maradhi ya kidingapopo (homa ya dengue), virusi vya Nile Magharibi, na majuzi zaidi, chikungunya. Sawa na maradhi haya, virusi vya Zika pia huenezwa na mbu.

Lakini kinyume na virusi hivyo vingine, hakuna chanjo dhidi ya Zika. Je, ni njia gani iliyopo ya kukabiliana na virusi hivi?

1. Kutumia dawa au mafuta ya kufukuza mbu

Ushauri wa kwanza kabisa ni kuepukana na mbu. Kituo cha Kudhubiti na Kuzuia Maradhi (CDC) nchini Marekani kinapendekeza watu wajipake mafuta yenye kemikali za kufukuza mbu kama vile N, N-diethyl-meta-toluamide (DEET) au picaridin.
Mafuta haya yanafaa kujipakwa mara kwa mara, kwa kufuata maagizo kwenye mikebe, au mtu anapoanza kuumwa na mbu. Mtu anafaa kujipaka baada ya kujipaka mafuta ya kukinga ngozi dhidi ya miali ya jua. Mafuta mengi ya kufukuza mbu ni salama hata kwa kina mama waja wazito, lakini ni vyema kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kuanza kuyatumia.

Image

2. Kuvalia mavazi ya kufunika mwili

Wataalamu pia wanakubaliana kwamba inafaa kuvalia mavazi yanayofunika mwili vyema. Mfano shati au nguo zenye kufunika mikono na pia suruali au long’i ndefu. Mavazi yanafaa kuwa mazito kuzuia mbu kufikia ngozi. Katika baadhi ya mataifa, mavazi huwekwa dawa maalum aina ya permethrin, ambao hufukuza mbu.
Iwapo utajipaka mafuta ya kufukuza mbu, usijipake na kisha kufunika maeneo uliyojipaka kwa nguo unazovalia.

3. Kuzuia mbu kuingia nyumbani

Ikiwezekana, wataalamu wanawashauri watu walale ndani ya nyumba zilizojengwa vyema na kuwekwa kinga ya kuzuia mbu kuingia. Usiku, lala chini ya neti zilizotibiwa.
Lakini usitahadhari usiku pekee kwani mbu aina ya Aedes aegypti, wanaoeneza virusi vya Zika, hupenda sana kuuma watu mchana.

Image

5. Kufunika taka

Maeneo ya kutupwa taka mara nyingi huwa na maji na hutumiwa sana na mbu kuzaana.
Ili kuzuia hili, ni vyema kufunika taka, hasa katika mifuko ya plastiki.
Tairi kuukuu na vitu vingine vya ujenzi pia vinafaa kuwekwa vyema, kwani sana huhifadhi maji ambayo yanaweza kutumiwa na viluwiluwi wa mbu.

6. “Kunyunyizia dawa”

Maafisa nchini Brazil, ambako virusi vya Zika vimeenea sana, wanatafakari wazo la kunyunyizia maeneo yaliyoathiriwa na virusi hivyo dawa ya kuua mbu.Hii inachukuliwa kama njia ya dharura kabla ya michezo ya Olimpiki, ambayo itaanza mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti.
Hata hivyo, kuna utata kwani njia hii inaweza kuwa na madhara mengine kwenye mazingira na pia kuathiri afya ya wakazi.

Image

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest