Wizara yazindua aina mpya ya Kondomu nchini

User avatar
Moderator 1
Site Admin
Posts: 13
Joined: Tue Jun 21, 2016 10:45 am
Contact:

Wizara yazindua aina mpya ya Kondomu nchini

Postby Moderator 1 » Mon Oct 03, 2016 11:38 pm

WIZARA ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua kondomu za kiume mpya aina ya Zana na kuzisambaza maeneo ya zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na za rufaa za mikoa ili zitolewe bila malipo kwa ajili kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na magonjwa yatokanayo na zinaa.

Katika utafiti wa viashiria vya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011/2012 kwa Watanzania uliweka bayana kwamba licha ya asilimia 69 ya wanawake na 77 ya wanaume miongoni mwa Watanzania watu wazima, wanafahamu matumizi ya kondomu. Hata hivyo alisema ni asilimia 27 ya watu hao wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu mara ya mwisho walipofanya ngono.

Uzinduzi wa Zana Kondom kitaifa ulifanyika mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo kwa mkoa wa Mwanza uzinduzi utafanyika kesho Jijini Mwanza ambapo aina hiyo ya kondomu itakuwa mbadala wa kondom za MSD zilizokuwa zikitolewa pia bure na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa.

Je? tofauti na vituo vya afya na zahanati, unafikiri sehemu za majumba ya starehe, hotel na gesti zitafikiwa ki-ufasaha na huduma hii bila wamiliki kutoza gharama yeyote?
Attachments
zana.jpg
zana.jpg (76.58 KiB) Viewed 2336 times

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest