Pumu kwa watoto - Uvutaji sigara kwa kina-baba moja ya chanzo

User avatar
Moderator 1
Site Admin
Posts: 13
Joined: Tue Jun 21, 2016 10:45 am
Contact:

Pumu kwa watoto - Uvutaji sigara kwa kina-baba moja ya chanzo

Postby Moderator 1 » Thu Oct 06, 2016 11:09 am

Ripoti ya utafiti kuhusiana na madhara ya uvutaji sigara imetathmini kuwa watu takriban milioni 150 wapo katika hatari ya kufariki kutokana na magonjwa yanayosababishwa na sigara.

Akiongea kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara Daktari Kemik alisema kuwa uvutaji wa sigara ni tishio kwa afya ya umma na kwamba ni lazima hatua zifaazo zichukuliwe kupunguza madhara yake.

Utafiti wao ulitathmini kuwa katika kipindi cha 2000 - 2024 watu milion 150 watapoteza maisha yao kutokana na magonjwa yanayosababishwa na uvutaji wa sigara. Daktari Kemik aliyesema kuwa sigara husababisha magonjwa, majeraha, matatizo ya kisaikolojia na hata vifo, aliongezea kuwa uvutaji wa sigara ni janga la kijamii.

Tahadhari kwa familia zenye watoto wachanga

Akitoa tahadhari kwa familia zenye watoto wachanga, Daktari Ersoz alisema kuwa athari za sigara huwa mara 5 zaidi kwa watoto. Mtoto mchanga anayelelewa katika nyumba inayovutwa sigara huwa mara 3 zaidi katika hatari ya kuugua magonjwa ya watoto. Hatari ya maumivu ya tumbo kama vile kolik huongezeka maradufu sawia na hatari ya kuambukizwa magonjwa katika mfumo wa kupumua.
Attachments
pic+marufuku-sigara.jpg
pic+marufuku-sigara.jpg (20.88 KiB) Viewed 1824 times

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest