Serikali: Hali ya chakula nchini ni nzuri

User avatar
Moderator 1
Site Admin
Posts: 13
Joined: Tue Jun 21, 2016 10:45 am
Contact:

Serikali: Hali ya chakula nchini ni nzuri

Postby Moderator 1 » Tue Jan 17, 2017 7:20 am

Image

LICHA ya Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kueleza hali ya usalama wa chakula duniani kuwa ni mbaya, lakini Serikali imesema kwa Tanzania hali ni nzuri kukiwa na uzalishaji wa chakula tani milioni 16 kwa mwaka huu tofauti na tani milioni 15 zilizozalishwa mwaka jana.

Akizungumza jana baada ya kuzindua ripoti ya FAO kuhusu hali ya chakula na kilimo kwa mwaka 2016, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka alisema mahitaji ya uzalishaji wa chakula nchini ni tani milioni 13.

Ripoti ya FAO imeainisha kuwepo kwa changamoto ya usalama wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ikisisitiza mbinu za uzalishaji wa chakula kubadilika kama ambavyo hali ya tabia nchi inavyobadilika.

“Tanzania hali ni nzuri, pia zipo baadhi ya nafaka ambazo uzalishaji wake ni mara mbili ya mahitaji, hivyo hali kitaifa imeendelea kuwa nzuri kufuatia kuwepo kwa ziada ya chakula,” alisema Dk Turuka.

Alisema kutokana na uzalishaji huo kuridhisha, nchi itakuwa na utoshelevu wa chakula kwa kiwango cha ziada kwa asilimia 123 ambapo kiwango cha chini kinachoweza kutia shaka ni asilimia 93 ambayo itaweza kuonesha hali ni mbaya.

Alisema mbali ya hali ya chakula kuwa nzuri nchini, zipo Halmashauri 43 zinakabiliwa na njaa jambo ambalo zinafanyika jitihada ili kuweza kupatiwa chakula, lakini idadi hiyo ikiwa ni pungufu kwa Halmashauri 69 zilizokumbwa na tatizo hilo kwa mwaka jana.
Source: Habari Leo

Alisema dunia inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula, hali inayohusishwa na mabadiliko ya tabianchi na kwamba ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu Mwaka 2030, ipo haja ya kuona namna ya kulifanyia kazi suala hilo.

Source: Habari Leo

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest