WIZARA YA AFYA YAKANUSHA UHABA WA CHANJO YA PEPOPUNDA

User avatar
Moderator 1
Site Admin
Posts: 13
Joined: Tue Jun 21, 2016 10:45 am
Contact:

WIZARA YA AFYA YAKANUSHA UHABA WA CHANJO YA PEPOPUNDA

Postby Moderator 1 » Tue Jan 03, 2017 9:50 am

Image

WIZARA YA AFYA YAKANUSHA UKOSEFU WA CHANJO YA PEPOPUNDA, Baada ya kuripotiwa taarifa kwamba kuna uhaba wa kinga za ugonjwa wa Pepopunda kwenye Hospitali za Dar es salaam, Leo Januari 2, 2017 Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa ufafanuzi kuhusu Chanjo hiyo na kueleza kuwa ipo akiba ya kutosha tofauti na ilivyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima leo Jumatatu ya tarehe 02 Januari 2017.

Wizara ya Afya imesema kuwa habari iliyotolewa na gazeti hili sio sahihi, na hata majina ya watu waliohojiwa kuhusu kuadimika kwa chanjo hiyo hawapo wizarani, na wengine wapo masomoni, ”hii ni taarifa ya zamani sana kimsingi imepitwa na wakati ambayo haikupaswa kutolewa na wahariri wa habari wangekuwa makini katika kufanyia kazi taarifa hii.

”Kwenye taarifa hiyo ametajwa Daktari kiongozi wa hospitali ya Amana, Stanley Dinagi, ambaye sasa hivi hayupo nchini, yupo masomoni. Pia ametajwa Mganga mkuu wa serikali Donald Mmbando ambaye hayupo katika wadhifa huo sasa imepita takribani miaka mitatu iliyopita”

Taarifa ya Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Afya, Nsachris B. Mwamaja imefafanua uwepo kinga hiyo katika wilaya kuu tatu za Dar es salaam.

Mkoa wa Dar Es Salaam una chanjo za Pepopunda zakutosha katika manispaa zake zote na umesambaza mgao wake kama ifuatavyo,

ILALA – Dozi 35,300 zilisambazwa Tarehe 06/12/2016 na mahitaji yao kwa mwezi Dozi 7,110.
TEMEKE – Dozi 33,000 zilisambazwa Tarehe 06/12/2016, mahitaji yao kwa mwezi ni Dozi 7,620.
KINONDONI – Dozi 11,000 zilisambazwa Tarehe 07/12/2016, mahitaji yao kwa mwezi ni dozi 9,210.

Msemaji huyo wa wizara ya afya amesema, “Kwa hivi sasa hakuna upungufu wowote wa chanjo ya pepopunda nchini. Tuna jumla ya dozi 599,000 katika bohari ya taifa, na tunatarajia kupokea shehena nyingine ya dozi 1,200,000 wakati wowote ili kuhakikisha kwamba hatuna uhaba wa chanjo hii.”

mligo
Posts: 0
Joined: Fri Jan 13, 2017 9:30 am
Contact:

Re: WIZARA YA AFYA YAKANUSHA UHABA WA CHANJO YA PEPOPUNDA

Postby mligo » Fri Jan 13, 2017 10:33 am

Hali si nzuri, vyema mambo yakawekwa wazi..

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest