Virusi vya Zika vyagunduliwa Tanzania

User avatar
Moderator 1
Site Admin
Posts: 13
Joined: Tue Jun 21, 2016 10:45 am
Contact:

Virusi vya Zika vyagunduliwa Tanzania

Postby Moderator 1 » Sun Dec 18, 2016 12:54 pm

Image
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR) imesema virusi vya Zika vimegunduliwa nchini humo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.

Kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti huo, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi vya Zika. Hata hivyo wizara afya nchini humo, imetoa taarifa ambapo inakanusha kuwepo kwa virusi hivyo.

"Kama nilivyoeleza mnamo februari 2016, ugonjwa huu bado haujaingia nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa Tanzania haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika," taarifa ya wizara ya afya imesema.
Wizara hiyo inasema uchunguzi uliofanywa na NIMR ulikuwa wa kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya Zika na Chikungunya.

"Matokeo haya bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina zaidi kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani," wizara imesema.

Dkt Mwele Malecela ameambia BBC kwamba kwa sasa serikali inaangazia kuzuia wajawazito wasiumwe na mbu ambao wanaaminika kueneza virusi hivyo.

"Bado tunajaribu kuangalia ni aina gani ya virusi vya Zika. Lakini hiyo ni dhahiri, tukizingatia kwamba mbu wanaoambukiza Zika wako nchini kwetu na mazingira yaliyoko nchini kwetu hayatofautiani sana na yale ya Amerika ya Kusini na nchi kama Thailand ambako ugonjwa huo unapatikana," amesema Bi Malecela.

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest